SERIKALI YAANZA HATUA ZA UTOAJI ELIMU YA UFUGAJI MASHULENI

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega amesema serikali imeanza hatua za utoaji elimu ya ufugaji kwa wanafunzi kwa kuanzisha Club zitakazowajengea uwezo wa ufugaji na kuwapatia ajira hata baada ya kumaliza masomo yao. Amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kukusanyia na kusindika bidhaa za maziwa kwa vyama